WAY

Monday, January 20, 2014

JUICE YA MACHUNGWA MKALI ALIEKUA ANAUNDA DIAMOND SOUND ALIA NA BEN KINYAINYA ASEMA ALIMPA LAKI NNE LAKINI HAKUPIGA NYIMBO YAKE NA MWISHO WA SIKU AKASEMA UZALENDO KWANZA SASA AIBUKA NA BAND YAKE AKIITA THE BEST 4 BYE 4

JINA la JUICE YA MACHUNGWA si geni katika masikio ya watu na hasa kama umeifuatilia diamond sound international ambayo iliweza kutamba na wimbo wake wa MAPENZI KITU GANI,ambapo kipande chake cha sasa umefika muda wa kuchezaaaaa............... na baada ya kufariki kwa aliekuwa mkurugenzi wa band hiyo ndipo band hiyo ilipoanza kusuasua na mwisho wa siku kugawanyiika na kuwa band mbili moja ikiitwa diamond musica origal ingine ikiitwa diamond musica nternational vijana classic lakini baadae ikashindwa kuhimili ndipo alipoweza kugawanyika rasmi na ndipo waliobaki kila mmoja akifanya kazi kivyake ambapo ALAIN MULUMBA akaweza kutoa kibinda nkoi remix ambayo alimshirikisha huyo huyo JUICE YA MACHUNGWA


SASA rapa huyo wa zamani wa DIAMOND MUSICA anasema watangazaji wengi wanajifanya wanainua muziki wa dansi lakini ndio wauaji wa muziki wa dansi akimtolea BENNY KINYAIYA na kusema alichokifanya hawezi kukisahau kamwe baada ya kutengeneza project yake na kuipeleka kwa media ndipo alipofika katika mikono ya benny kinyaiya alipomwambia ampe laki nne kwa ajili ya promotion ndipo alipoitafuta kwa udi na uvumba na kuipata kisha kumpa benny lakini mwisho wa siku nyimbo yake haikupigwa wala kufanyiwa promo kama alivyoahidiwa na mwisho wa siku ndipo alipoamua kumtafuta kwenye simu na alichoambuliwa ni matusi na dharau na kuambiwa kuwa kwa sasa wanafanya uzalendo kwa wanamuziki wa kitanzania kwa vile yeye mcongo basi hawezi kupewa promo na mwisho wa siku nyimbo hiyo mpaka sasa ameamua kutoipeleka kwengine  na sasa ameamua kufanya album na baada ya hapo aweze kuizindua,

ILA juice ya machungwa kwa sasa amesema kuwa ameanzisha band yake inaitwa THE BEST 4 BYE 4 ambayo kwa sasa ameshaanza kufanya show baada ya kushindikana kwa kuanzishwa kwa band ya LA MUSICA BAND kutokana na mdhamini kulega lega na kushindwa kusimimamia kikamilifu uanzishwaji wa band hiyo na kusisitiza kutoka kwenye band yake mpka mwezi wa tano atakua ameshakamilisha album yake

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...