WAY

Thursday, January 23, 2014

Baadhi ya mabasi yanayofanya safari zake kupitia barabara ya Dodoma hadi Dar es Salaam yamesitisha safari hizo kutokana na kuvunjika kwa daraja la eneo la Dumila mkoani Morogoro.

 Baadhi ya mabasi yanayofanya safari zake kupitia barabara ya Dodoma hadi Dar es Salaam yamesitisha safari hizo kutokana na kuvunjika kwa daraja la eneo la Dumila mkoani Morogoro.
Kutokana na mabasi hayo kukataisha safari zake  abiria wanaopita njia hiyo wamepata wakati mgumu kutafuta usafiri wa kufika huko, huku nauli za mabasi zikiwa juu.
Akizungumza na kituo hiki, Wakala Mkuu wa mabasi katika stendi ya Mkoa wa Dodoma, Rashidi Zuberi amesema baadhi ya mabasi yamekatisha safari zao lakini mengine yanaendelea na safari kama kawaida kupitia njia ya Iringa.
“Asubuhi mabasi yote yalikuwa yanapitia Iringa kwa nauli ya Sh. 30,000 badala ya Sh. 17,000 hadi Sh. 22,000 lakini baadae tulivyoona mabasi ya Mwanza yakipita njia ya Kilosa na mabasi mengine yameanza kupitia njia hiyo ya Kilosa.
“Hata hivyo mabasi kama Shabiby na Kimbinyiko naona wenyewe wameamua kusitisha safari zao labda wanahofia ubovu wa barabara ya Kilosa,” alisema
Akizungumzia hali hiyo, mfanyakazi wa Ofisi ya Mabasi ya Kampuni ya Shabiby, Mushi Abdul amesema  kuwa mabasi ya Shabiby yalifanya safari zake, mwisho basi la saa tatu asubuhi kwa kupitia njia ya Kilosa.
“Safari za mabasi mengine zimesitishwa na tiketi zilizokuwa zimeuzwa jana kwa basi la saa tano tumewarudishia abiria fedha zao,” alisema
Hata hivyo kulikuwa na idadi ndogo ya mabasi ambayo yalikuwa yanapakia abiria kwa siku ya leo tofauti na siku nyingine.
Akizungumzia adha hiyo ya usafiri abiria aliyekuwa anatafuta usafiri wa kwendaa Jijini Dar es Salaam, Michael Lembu alisema tangu amefika kituoni hapo anatafuta usafiri lakini bado hajapata.
“Tunaiomba Serikali ifanye haraka kujenga daraja lililobomoka ili safari zirejee kama kawaida,” alisema.
Kwa upande wake  mmoja wa wakala wa mabasi katika stendi hiyo ambaye hakutaka  kutaja jina lake alisema nauli ya Dodoma hadi Dar es Saam kwa njia ya Kilosa imepanda kutoka Sh. 17,000 hadi Sh. 20,000 na kwa mabasi ya Luxury nauli ni Sh. 30,000.
“Hata hivyo barabara ya Kilosa ni mbaya kuna baadhi ya magari ambayo yana matairi mawilimawili hayawezi kupita,” alisema.
Mwisho.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...