MASASI 20/1/2014
Wazazi
wilayani MASASI wametakiwa kuipa eilimu kipaumbele,sambamba na kuacha mitazamo hasi
na potofu.
Hayo
yameelezwa na mwalimu mkuu wa shule ya
msing CHIGUGU wilayani Masasi Bw.YOHANA ABUNUAS wakati akizungumza na safari
radio ofisini kwake.
ABUNUAS
amesema miongoni mwa changamoto kubwa wanazo kumbanana nazo wilayani Masasi ni
mwamko mdogo wa wazazi wa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao,kama wazazi
wataipa elimu kipaumbele elimu itakua mkombozi kwa vijana wengi hapa nchini.
Aidha amelaani
kitendo cha baadhi ya wazazi na walezi kupuuza umuhimu wa elimu na kushindwa
kupeleka watoto wao shule pasipo sababu yeyote ya msingi.
Katika Hali
isiyo ya kawaida shule ya msingi CHIGUGU hadi kufikia January 17 mwaka huu
jumla ya watoto 35 pekee ndio wameandikishwa darasa la kwanza ,huku matarajio
ya shule hiyo ikiwa ni kuandikisha watoto 135 wasajiliwe darasa la kwanza.
Kufuatia
hali hiyo ABUNUAS amewahimiza wazazi na walezi wenye watoto wanao stahili
kuingia darasa la kwanza wapelekwe shule
kwani hiyo ni haki yao ya msingi.
BEATRICE
RIWA
0 comments:
Post a Comment