WAY

Tuesday, January 21, 2014

JE WAJUA? ALLY CHOKI ILIMLAZIMU KULALA CCM SEHEMU ZA KUOGESHEA MAGARI WAKATI ANATAFUTA KUTOKA KIMUZIKI ASEMA HATA BAADA YA KUMALIZA SHULE ALIEDNELEA KUTUMIA UNIFORM ILI AWEZE KUPANDA DALADALA KWA BEI RAHISI AKAPIGE MIZIKI DAR KUTOKA KIBAHA nNA LEO NDIO MKURUGENZI WA EXTRA BONGO

Leo katika je wajua mkurugenzi wa EXTRA BONGO le kamarade ally choki amesimuli alipotokea katika muziki na changamoto alizokutana nazo katika muziki ni pamoja kuweza kulala katika sehemu za maegesho ya magari tena usiku mnene na kuamika asubi sana kuendelea na harakati zingine mpka alipoweza kupata band katika miaka ya 87 na kuanza kuimba na mwisho wa siku kuweza kuelekea hadi nchini kenya lakini hata hivyo kitu kingine anachokikumbuka ni kuweza hata baadaa ya kumaliza shule aliweza kuendelea kuvaa uniform ili aweze kupanda daladala kwa bei ya mwanafunzi ali aweze kwenda kufanya miziki mjini dar kutokea kibaha

Akizungumzia siri ya mafanikio yake katika muziki amesema inatokana na juhudi pamoja kuupenda muziki na ndio maana mpka leo ameweza kujielewa na kuweza kusimama na band yake mwenywe ingawa kuna wenzake walitoka pamoja huko ila kutokana na mipango wengine wameshindwa kufanya kama alivyofanya yeye ila anasema malengo aliyoyaweka toka aanza muziki ndio yaliyomfikisha mpka alipo hii hii leo.
 
   
ALLY CHOKI amelia sana na wakurugenzi wa baadhi ya band kwa kuwa wabania wanamuziki kwa kutaka wasipate kama wanavyopata wao yaani viongozi wengi hawapendi kuona mwanamuziki wake anaendesha gari ya thamani zaidi yake kitu ambachokwa mujibu wa ally choki ni wivu usiokuwa na maendeleo au hata mwanamuziki akitaka kufanya kazi yake njee ya kundi au kwenda kutafuta maisha au kumjali mwanamuziki baada ya kuungua nacho ni kitu ambacho anasema wakurugenzi wanatakiwa kutoa vipaumbel zaidi.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...