WAY

Wednesday, November 14, 2012

DK CHENI APANIA KUTAFUTA MRITHI WAKE KATIKA MIKOA YA KUSINI MBIONI KUFANYA FILAMU STAR SEARCH MTWARA NA LINDI AAHIDI KUFANYA NAO KAZI BEGA KWA BEGA KWA HUKO NDIO KWAO,MBIONI KUINGIZA SOKONI FILAMU YAKE YA MAJANGA

MSANII nguli wa maigizo tanzania ambae anatamba sana katika ulimwengu wa bongo filamu kwa sasa lakini alianzia mbali DK CHENI amesema kwa sasa yupo kimya kutokana na kuzongwa na kazi nyingi za biahara yake anazo fanya kwa sasa lakini amesema mwezi wa kumi na mbili ataingiza filamu moja kabambe itakayoizidi one by one ambayo ameipa jina la MAJANGA ambapo ndani yake kazungumzia vitu vingi ikiwemo mmomonyoko wa maadili katika baadhi ya familia kwa sasa watoto karibu wote kuharibikiwa na hadi wazazi nao kukosa maadili.
                                            DK CHENI AKIWA NA IRENE UWOYA
DK CHENI amesema kwa sasa anauchungu sana na kuwainua upcoming artist hasa kutoka mikoani ambapo ataanza kazi ya kuwasaka kwa kuanzia mikoani akizan mkoa wa LINDI NA MTWARA ambapko anasema ndio asili yake hususani mkoani kilwa ndipo anapotoka yeye ila kwa kutafuta vipaji ataenda hadi kwenye wilaya mbalimbali za mtwara na lindi ili kusaka vipaji ambapo ana imani kabisa ataweza kuppata mrithi wake pindi atakapoa achana na ulimwengu wa sanaa za maigizo.
 AIDHA CHENI amesema licha ya kusaka vipaji hivyo mikoani pia ataweza kuwagharamia kila kiti na kuweza kufanya nao kazi moja amabayo itakua kabambe kabisa na kuweza  kuwatoa waliko na kuwa moja kati ya waigiaji wakubwa kabisa kupitia yeye hata hivyo cheni kwa sasa ansema yupo kwenye mchakato wa kuingiza filamu yake ya MAJANGA sokoni ambayo ansema itakua ni kiboko.
                                         DK CHENI AKISALIMIA NA RAIS KIKWETE
                                 DK CHENI NA SAJUKI NDANI YA ONE BY ONE

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...